Ommy Dimpoz nae kaamua kutoboa pua na kusema haya

0

Kuna uwezekano mkubwa hii style mpya ya wasanii wa kiume kutoboa pua ikaenea kwa wasanii wengi zaidi. Ilianza kwa msanii Chid Benz ambae mara baada tu ya kuonekana katoboa pua ilikua gumzo sana sio tu magazetini hata mitandaoni huku wasanii wengi wakipingana na maamuzi yake.

Itakumbukwa pia kua Diamond Platnumz alifikia hatua hadi ya kumuimba Chid kua katoboa pua ila cha kushanaza mwaka huu nae Diamond katoboa pua. Ishu ya Diamond kutoboa pua ishasambaa sana ila mpya kwa sasa ni Ommy Dimpoz nae kutoboa pua!!!

Imenaswa video ikimwonyesha Ommy Dimpoz akiwaonyesha mashabiki wake kua nae katoboa pua, hadi akatoa heleni ya sikioni na kuiweka puani. Unaweza ona video hiyo hapa chini…

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here