Timu Wema Wamtosa Wema Sepetu Mapokezi ya Van Vicker

0
wema sepetu na van vicker

Sio kawaida kwa mwanadada Wema sepetu kupokea mgeni katika viwanja vya ndege kama ilivyotokea alfajiri ya leo kwa kuosekana kwa umati wa watu.Kama alivyokuwa akitoa taarifa ya ujio wa msanii huyo mkubwa kutoka Nigeria, alisema kuwa msanii huyo atakapo fika atakuja kupokelewa na watu mbalimbali kwa sababu ni mgeni wake.

Wema amekuwa moja ya watu wanaomamini kuwa na mashabiki wengi sana na kwa kuthibitisha hilo, utakumbuka ilivyokuwa wakati wa kumpokea mwanadada Omotola ambae aliwahi kuja Tanzania kwa mwaliko wa mwanadada Wema Sepetu jinsi ambavyo alipokelewa na watu wengi hasa Team Wema .

Hii inaweza kuleta maswali mengi sana kuhusu mashabiki wa Wema hasa wale wanaojiita Team wema kuwa walikuwa wapi kumpa sapoti msanii wao kama kweli wao ni Team Wema au ndio mapenzi yameanza kuisha.

Hali ilivyokuwa uwanja wa taifa ni tofauti na ile amsha amsha ya Wema kila anapokuwa na mgeni katika viwanja hivyo, hata hivyo siku ya shughuli bado hivyo tunaamini kuwa watajitokeza wengi kumsapoti katika siku yake ya kuzaliwa lakini pia katika uzinduzi wa filamu hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here