Stereo Feat G Nako – Sana (Lyrics)

0

 EXCLUSIVE  Stereo Feat G NakoSana (Lyrics) | Mistari

Stereo Feat G Nako - Sana (Lyrics)
[Verse 1 – Stereo]
Kila napochana wanapiga makofi sana
Baby anasema mimi ni mkorofi sana
Ukweli ni kwamba namkubali Koffi sana
Nilioza meno kwa kupenda pipi toffee sana
Siwezi kusubiri muda unayoyoma sana
Darasani vilaza ndo wanaosoma sana
Maza halali usiku dingi anakoroma sana
Ukitembea peku miba itakuchoma sana
Zikija defender tunatandikwa marungu sana
Wengine hupasuka, wengine manundu sana
Ukifanikiwa utapigwa majungu sana
Kuna watu wakilewa wanaongea kizungu sana
Siku hizi wasichana wanavaa vikuku sana
Watoto wa sekondari wananyoa viduku sana
Hali inatisha sana
Wenzangu wenye smartphones kazi ni ku-chat na kutuma picha sana
Nimepanga ghetto Tandale kuna wizi sana
Usiku na mchana silali usingizi sana
Bodaboda kwenye lami wanapiga mbizi sana
Nikimuelewa ticha maswali siulizi sana

[Pre-Hook – G Nako]
Neno langu somo likuguse
Neno langu somo usilitupe
Wa moto kama fire usiniguse
Usizingue ukae usinirushe
[Hook – G Nako]
Wanimanyile, wanimanya
We mwana wanimanyile, wanimanya
Wanimanyile, wanimanya
We mwana wanimanyile
Iyeeh, jee, jeh jee
[Verse 2 – Stereo]
Hatuli bata tunakula mbuzi sana
Makondakta wanahonga wanafunzi sana
Masista duu wanachuna mabuzi sana
Utafilisika ukiendekeza matanuzi sana
Hatuvai moka, tunavaa mabuti sana
Siku hizi tunavaa boxer, hatuvai chupi sana
Wenye mali za majini udi mtafukiza sana
Dr. Magufuli huja kwa kushtukiza sana
Ukiwa na demu mkali jiandae sana
Kupata stress na pressure, usishangae sana
Atamendewa sana, utamegewa sana
Ukikosa pesa, mapicha picha utachezewa sana
Katiza Kona baa, wanyama wengi sana
Ukisikia “pah!” huyo jamaa halengi sana
Sishabikii Yanga, mi mnyama Simba sana
Mbona mahousigeli wanapata mimba sana?
Sio ugali, wapemba wanapenda wali sana
Wasanii wa Bongo hawapendi kusali sana
Hatufanyi shopping za kishua sana
Vichwa na miguu ya kuku ndo tunanunua sana
[Pre-Hook – G Nako]
Neno langu somo likuguse
Neno langu somo usilitupe
Wa moto kama fire usiniguse
Usizingue ukae usinirushe, eh
[Hook – G Nako]
Wanimanyile, wanimanya
We mwana wanimanyile, wanimanya
Wanimanyile, wanimanya
We mwana wanimanyile
Iyeeh, jee, jeh jee
[Outro – Stereo & G Nako]
Wali panya, wali nyanya
Wali nyama, eh yeah, wali panya
Eh bwana, bwana wee
Ai, Mashindoni bwana wee
Ee singa singa, eh De Kankara
Ee bwana weeh, Kiri Record bwana
Ai!

Download : Stereo Feat G Nako – Sana

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here