Nikki Awapeleka Wasanii Darasani

Msanii wa HipHop anayetamba na kundi la Weusi, Nikki wa Pili ametoa ushauri wake juu ya suala kuongezeka kwa wasanii wengi wa Bongo Fleva ambao wana umaarufu mkubwa kuliko kipato chao.

Nikki amesema kuwa ili kubadili muonekano wa wasanii na kuwafanya kuwa na kipato, wanahitaji kupewa masomo ya mauzo, masoko na jinsi ya kukuza (brand) majina yao.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Nikki wa Pili ameandika, "kuibadili sanaa kuwa fedha ni hatua ngumu, iwe uchoraji, uchongaji, uandishi, muziki, sarakasi nk, wasanii wengi mno wamebaki na sanaa zao kama hobi na sio kitu cha kupatia kipato. Somo la marketing (masoko), sales (mauzo), branding (kujikuza) na huduma kwa wateja katika eneo la sanaa ni muhimu mno."

Kauli hiyo inakuja huku kukiwa na mjadala mkubwa na wa muda mrefu juu juu ya hali za kimaisha za wasanii kuwa chini tofauti na ukubwa wa majina yao sehemu mbalimbali duniani.This is Bongo Exclusive Official Website (Everything Exclusive) you can follow our social network pages or email us: bongoexclusive@hotmail.com

Become Our VIP Subscriber, Jiunge Sasa!

 
Top